Dar es Salaam. Ally Chande (16), mkazi wa Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam aliyepotea Julai 14, 2019 akiwa anaogelea katika Bahari ya Hindi amekutwa amekufa ufukweni karibu na hoteli ya Sea Cliff.
Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kambangwa alipotea Jumapili akiwa katika ufukwe wa Coco.
Ilielezwa Chande aliingia kuogelea katika Bahari ya Hindi eneo hilo, hakuonekana tena hadi jana jioni Jumanne mwili wake ulipokutwa ufukweni.
Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne Julai 16, 2019 baba mdogo wa mtoto wa Ally, Mohamed Chande amesema walipata taarifa za kupatikana kwa mwili katika eneo hilo na walipoenda kufuatilia waliutambua.
“Kuna mtu tunaishi naye huku jirani anafanya kazi huko jioni alitupigia simu kuna mwili umeonekana, tulikwenda kuangalia na kutambua kuwa ni Ally.”
“Ameharibika inaonekana amekunywa maji mengi sana, ila kwa sasa tumewaachia polisi wamalize taratibu zao kabla hawajatukabidhi mwili kwa ajili ya mazishi,” alisema Mohamed.
Pia Soma
- Anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma moto ashikiliwa polisi
- Umahiri wa Faru Rajabu unavyoleta matumaini ya kuongeza idadi yao Tanzania
- UBISHI MPYA; Zari na mama Diamond nani mkubwa?