Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyepata PhD na miaka 75 kusaidia wanawake

Phdpic Aliyepata PhD na miaka 75 kusaidia wanawake

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Bibi Kezia Mashingia, mwenye umri wa miaka 75, amehitimu shahada ya uzamivu (PhD) katika chuo kikuu cha kikatoliki Mwenge (Mwecau)

Dk Mashingia ambaye ameonekana kuwa mwenye furaha na bashasha, amegeuka kuwa kivutio kwa wahitimu wenzake na watu waliofika kushuhudia mahafali hayo.

Jumla ya wanachuo 857 wamefuzu masomo yao katika chuo kikuu cha kikatoliki Mwenge (Mwecau) na kutunukiwa Astashahada, Stashahada na shahada mbalimbali ambapo wa PhD walikuwepo watano,

Akizungumza leo Novemba 27, Mashingia ambaye ameweka historia ya kupata PhD akiwa na umri mkubwa, amesema anakusudia kuanzisha mfuko (Foundation) kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike na wanawake kupata elimu.

Amesema lengo lake la kupata elimu katika umri huo ni kuhamasisha vijana hususani wa kike na kina mama kupata elimu na kwamba ataanzisha mfuko wa kusaidia kundi hilo ili waweze kupata elimu.

"Ninawaasa wanawake na wasichana, elimu haina mwisho, wasikate tamaa na changamoto zozote wanazozipata, wasome kwa sababu inawezekana pamoja na majukumu mengi waliyo nayo, maana mimi nimesoma baada ya kuzaa watoto saba na kuwa na familia" amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live