Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyenusurika kuuawa Kibiti aomba msaada

46710 Kibiti+pic

Thu, 14 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rondo, kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani, Michael Buchayandi ameomba msaada wa matibabu ili aweze kunusuru jicho lake moja.

Buchayandi alishambuliwa usiku wa Juni 27 mwaka 2017 kwa kupigwa risasi, rungu na kusababishiwa majeraha kadhaa ikiwemo kuharibiwa macho yake yote huku nyumba yake ikichomwa moto na watu waliowaua viongozi mbalimbali wa mkoa wa Pwani.

Buchayandi ametoa kilio hicho leo Alhamisi, Machi 14, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Licha ya muda mrefu kupita tangu ashambuliwe Buchayandi amelalamika bado anapata maumivu makali kwenye macho yake na muda wote yanatoa machozi.

Mke wa Buchayandi, Selina Mponye amesema katika mizunguko yao kwenye hospitali mbalimbali wamepewa matumaini upo uwezekano wa jicho moja kupona.

Kufuatia hali hiyo mbunge wa viti maalum (CCM) Subira Mgalu amejitolea kushirikiana na familia hiyo kutafuta wataalam watakaowezesha kupata matibabu ya kunusuru jicho hilo.

“Nataka tuanzie hospitali madaktari waangalie kama kweli uwezekano wa kuona jicho moja upo ni heri tumsaidie kwa kuanzia hapo, hilo likishathibitishwa na wataalam tuanze sasa kuhangaikia matibabu, niwaombe Watanzania wote kwa ujumla tuwe pamoja katika hili,” amesema Mgalu ambaye pia ni naibu waziri wa nishati.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz