Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemwandikia barua Rais Samia apewa milioni tano

Kijana Samia Aliyemwandikia barua Rais Samia apewa milioni tano

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amempatia mtaji wa biashara na fedha za kujikimu kijana Yassin Said mwenye ulemavu wa ngozi, baada ya kijana huyo kumwandikia barua akiomba kuwezeshwa kiuchumi.

Yassin ambaye amepitia masaibu katika maisha yake, amekabidhiwa fedha hizo kiasi cha TZS milioni 5.3 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kwa niaba ya Rais Samia.

Makalla amemsisitiza amesisitiza kutumia fedha alizopatiwa kujiimarisha kiuchumi ili lengo la Rais la kutoa fedha hizo liweze kutimia.

Kwa upande wake Yassin amemshukuru Rais kwa msaada aliopatiwa na kuahidi kuzitumia pea hizo kwa lengo lililokusudiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live