Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyempiga ngumi mbili kikongwe aachiwa huru

Thu, 23 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuachia huru mshtakiwa Neema Athuman (60) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya jinai namba 180/2018 akidaiwa kumpiga  Amina Abdallah (80).

Katika kesi hiyo, Neema anadaiwa kumpiga ngumi mbili Amina katika ugomvi uliotokea baina yao.

Hakimu Mkazi, Catherine Kihoja alitoa hukumu hiyo leo Alhamisi Mei 23, 2019  baada  kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi na kumuona mshtakiwa huyo hana hatia.

Hiyo ilitokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka hilo pasipo kuacha shaka yoyote.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wa Serikali, Grace Lwila.

Katika kesi hiyo Neema anadaiwa Februari 23,2017 Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam alimpiga Amina kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz