Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja mkazi wa Mikumi anayejulikana kwa jina la Hassan Mangoma amejisalimisha kwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni akidai kuwa alikuwa muhalifu aliyeshiriki ujambazi na wizi sehemu mbalimbali lakini kwa sasa ameamua kuacha tabia hiyo nakuamua kujitafutia Ridhiki kwa njia ya halali.
Hassan alifika katika mkutano wa hadhara wakati Waziri Masauni akizungumza na wananchi wa mikumi Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro na kuomba kueleza changamoto zake na ndipo alipofichua siri hiyo kuwa alikuwa mhalifu wa ujambazi na wizi.
Kufuatia hayo Waziri Masauni akampongeza kwa kuacha uhalifu na kuamua kujitafutia fedha zake kwa kazi za halali.
Pia, Waziri Masauni pamoja na viongozi wengine wengine walichanga fedha kiasi cha 200,000 na kumkabidhi ikiwa ni kutoa motisha kwa watu wengine kuacha uhalifu.