Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa RPC Zanzibar aswaliwa, anazikwa Mwanakwerekwe

61884 Maziko+pic

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Wananchi na askari na maofisa wa Polisi tayari wamefika katika Msikiti wa Kibweni kwa ajili ya kuisalia maiti ya aliyekua kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Aziz Mohamed Juma.

Mohammed ambaye amefariki dunia leo  Jumapili Juni 9, 2019, maiti yake imekutwa ikining’inia kando ya nyumba yake na atazikwa  makaburi ya Mwanakwerekwe yaliyopo mjini hapa.

Wananchi wengi wanaonekana kuwa na huzuni na kushindwa kuamini kilichotokea baada ya taarifa za kifo kuelezwa  kuwa ni za kujinyonga.

Awali, Kamanda wa Polisi Zanzibar, Mohamed Hassan Haji aliliambia Mwananchi kuwa kifo cha ofisa huyo si cha kawaida.

Hata hivyo, alisema licha ya uwapo wa tetesi kuwa amejinyonga nje ya nyumba yake huko Kijichi, lakini alisema hawezi kueleza kwa kina taarifa hizo kwa sasa kwa sababu bado mapema.

Alisema wanachokifanya sasa ni uchunguzi na wakibaini sababu watatoa taarifa.

Pia Soma

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi kutoka Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, Dk Msafiri Marijani amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kifo cha askari huyo si cha kawaida ingawa taarifa zaidi watatoa wahusika.

Tayari zilichukuliwa sampuli za damu kwa uchunguzi zaidi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz