Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejipanga kuuza supu Fiesta asimulia anavyohaha kusaka wateja

28692 Kongoro+pic TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Sinza Mori jijini Dar es Salaam,  Beatrice Msacky, ameeleza namna alivyopata hasara ya Sh3 milioni kutokana na kutofanyika kwa tamasha la Fiesta.

Mjasiriamali huyo mwenye mtoto mmoja wa  miezi minne amesema amehaha kupunguza hasara kwa kuwa fedha hiyo ameitoa katika biashara yake ya mapazia.

Beatrice ambaye ujumbe wake wa kusaka wateja umesambaza katika mitandao ya kijamii, amesema ili kurudisha hata nusu hasara ya fedha aliyoitumia kwenye kununua  kongoro, ulimi na mkia,  ameamua kuuza kwa hasara,

Amesema amejiuliza maswali mengi sababu za tamasha hilo kunyimwa kibali, kuhoji sababu za mamlaka husika kutositisha tamasha hilo mapema.

 

 “Hapa nilipo nimechoka dada, hata kula sijala tangu asubuhi na nina mtoto mdogo anatakiwa kunyonya,” amesema.

“Mbaya zaidi nimekodi watu sita wa kunisaidia kufanya kazi hiyo na wengine nilishawalipa kianzio, inabidi tu niuze nusu hasara na wengine wananipigia simu niwapelekee walipo.”

Ameongeza, “Hebu fikiria nimemuacha mtoto wangu wa miezi minne saa tisa usiku na kwenda kununua vitu machinjioni, nimerudi nimeviandaa nimekodi  na sahani na vyombo vingine ikiwemo majiko.”

“Yote haya nilikuwa nikiyafanya nikijua hela yangu itarudi lakini matokeo yake ni haya, wala siwalaumu Clouds kwa kuwa najua na wao huko walipo wamechanganyikiwa na wanaliana gharama ambazo wameingia.”

Supu ya kongoro aliyopaswa kuuza Sh3,000 hivi sasa anauza kwa Sh1,500.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz