Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyehama Chadema achaguliwa Naibu Meya Iringa

16151 Pic+meya TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Hamid Njovu amemtangaza Joseph Lyata, kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa.

Lyata amegombea nafasi hii kwa mara ya pili, baada ya kuhama Chadema na kuhamia CCM. Alikuwa Naibu Meya kupitia Chadema. Alikuwa Diwani wa kata ya Kwakilosa na Mwenyekiti wa madiwani kanda ya Nyasa.

Akitangaza matokeo hayo leo Septemba 7, Njovu amesema Lyata amepata kura 15, na mpinzani wake Sevline Mtitu amepata kura 13.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika leo katika ukumbi wa Manispaa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la madiwani ambapo jumla ya wajumbe 28 walipiga kura.

Awali akijinadi kabla ya zoezi la upigaji kura Lyata ambaye alikuwa akiomba nafasi hiyo kwa mara nyingine amesema akichaguliwa kuwa Naibu Meya atahakikisha anarudisha ushirikiano na kuwa msaada mkubwa kwa wananchi kutokana na uzoefu alionao katika kuendesha baraza.

Lyata amesema wakati akiwa Naibu Meya kupitia Chadema alikuwa na ushirikiano mzuri na madiwani na viongozi wa Serikali katika kuwawakilisha wananchi.

"Kazi ya Naibu meya ni kumuwakilisha meya na mwananchi hata kama wapo, kwa hiyo nitaendeleza ushirikiano huo na kuhakikisha baraza linakuwa na amani na hali katika uendeshwaji wake,"amesema.

Amesema atahakikisha anabuni miradi ya maendeleo, vyanzo vya mapato na kutafuta wawekezaji ili kuleta maendeleo katika halmashauri ya Iringa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz