Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyegongwa namwendokasi anaendelea vizuri - MOI

Mendok.jpeg Aliyegongwa namwendokasi anaendelea vizuri - MOI

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusambaa kwa video ya CCTV ikionesha ajali ya Basi la Abiria la “Mwendokasi” jana, Watu wengi wamejikuta kwenye huzuni huku baadhi yao wakihofia uhai wa Mtembea kwa miguu huyo ambaye alionekana akigongwa na Basi hilo na kubanwa ukutani.

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha Taasisi ya tiba ya mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), Patrick Mvungi amesema kuwa majeruhi huyu ambaye bado hawajamtambua majina yake, yupo kwenye Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na anaendelea vizuri kwa sasa.

“Wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba wanamrudisha awe vizuri lakini pia kwa sasa hali yake inaendelea vizuri, alishafanyiwa upasuaji kwa sababu ameumia mguu, amevunjika mfupa wa paja lakini pia amevunjika mkono mmoja ambapo Wataalamu wameshafanya upasuaji kwenye upande huo na pia aliumia kichwani... Wataalamu wameshamuhudumia anaendelea vizuri”

“Ni matarajio yetu kwamba siku chache zijazo ataweza kuamka na atatuambia yeye ni nani na ametokea wapi lakini tutumie nafasi hii kuwatangazia Watanzania kama kuna ndugu yenu hamumuoni inawezekana ni huyu, waje wamuangalie kama wanamfahamu ili waweze kushirikiana na sisi kwenye kumuhudumia.

“Kutokana na maelezo ya Wataalamu na jinsi tunavyomuona pale wodini kitu ambacho hawezi kufanya sasa hivi ni kuongea tu, hilo la kutokuwa na kumbukumbu linaweza kuwa kwa asilimia ndogo.

"Ni kwa sababu aligonga kichwa na wataalamu wanasema haikuwa na impact kubwa kwenye ubongo wake kwa hiyo sidhani kama anaweza akawa na changamoto kwenye kumbukumbu,” amesema Patrick Mvungi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live