Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyegongwa na mwendokasi yupo ICU

Mwendokasi Ajali Icu (600 X 388) Aliyegongwa na mwendokasi yupo ICU

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya tiba ya mifupa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imesema Mwanaume aliyeonekana akigongwa na Basi la abiria “mwendokasi” Jijini Dar es salaam jana, amelazwa Hospitalini hapo kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano cha MOI Patrick Mvungi amesema kuwa Mtu huyo wamempa jina la ‘UNKNOWN’ kwa sababu mpaka sasa hawana taarifa zake rasmi.

Mvungi ameongeza kuwa mpaka sasa Mtu huyo ambaye amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani hawezi kuongea lakini anafungua macho

Chanzo: www.tanzaniaweb.live