Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyechomwa sindano kimakosa, vidole vyaoza, sasa kukatwa mkono

Ester Mkombozi.jpeg Aliyechomwa sindano kimakosa, vidole vyaoza, sasa kukatwa mkono

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke ajulikanaye kwa jina la Ester Mkombozi mkaazi wa Kata ya Kimandolu Arusha ameoza sehemu ya vidole vyote vya mkono wa kushoto baada ya kuchomwa sindano katika duka la dawa katika eneo la Ngulelo jambo ambalo limepelekea kukatwa vidole vyote.

Akizungumza Ester amesema kuwa Machi 30, mwaka huu alienda katika Duka la Dawa kwa sababu alikuwa na tatizo la UTI ndipo akachomwa sindano jambo ambalo alianza kusikia maumivu pale pale na kupelekea mkono wake kuuma mara kwa mara na kuona Vidole vinabadilika rangi mpaka kupelekea kuoza kabisa

Ester ambaye kwasasa anaendelea na matibabu katika Hosptali ya Rufaa ya Mount Meru mkoa wa Arusha, amesema kuwa mnamo Machi 20, 2023 alihisi hali ya kutojisikia vizuri kiafya na kuamua kwenda kupata huduma katika Phamasi iliyopo eneo la Ngulelo Wilayani Arumeru.

Baada ya kufika na kupima na kuambiwa anaumwa ugonjwa wa UTI alichomwa sindano katika mkono huo ambayo aliambiwa niyakutibu ugonjwa huo, na hatimaye maumivu makali yalianza bila kukoma

“Nilienda duka la dawa nikiwa nasikia maumivu makali, nikapima na majibu yalitoka kwamba nina UTI, nikaambiwa nianze dozi ya sindano, nikaanza siku ile ile. Baada ya kuchoma, mkono nikaanza kuuma sana papo hapo.

“Nikatoka siku ya pili yake, nikaenda kwenye duka jingine na kile kichupa cha dawa, nesi akaniambia hii dawa haina matatizo lakini hakupaswa kukuchoma mkononi, alipaswa kuchoma kwenye makalio. Nilienda nyumbani maumivu makali sana, sikulala, kesho yake nikarudi pale nikakuta pamefungwa.

“Nikarudi kesho yake nikapewa dawa ya kuchua na vidonge vya kumeza lakini mkono uliendelea kuvimba, usiku kucha silali nakesha mkono unauma. Nilipokuja Mount Meru daktari akaniwekea drip ya dawa, uvimbe ukaisha ila vidole vikawa vyeusi sana. Vidole vikaendelea kulika na sasa havina mawasiliano kabisa.

“Baadaye madaktari waliponifanyia uchunguzi wakasema kwa hali niliyo nayo vidole vimeshaharibika, hakuna namna nyingine zaidi ya kufanyiwa upasuaji na kuvikata. Sasa hivi naskia amefunga lile duka lake na amekana kwamba hanijui wala hajawahi kunihudumia, sikutegemea kwa hili lililonitokea.

“Nilishazoea nasuka ili nipate mahitaji yangu, lakini sasa hivi sijui naenda kuanzia wapi na mkono mmoja? Nina watoto wawili sina baba wala mama, naomba mnisaidie namba yangu 0788618073 jina ni Sauda Ismail,” alisema Ester.

Akizungumza Doka Amani Kiruu amesema kuwa Mei 1, walimpokea mgonjwa huyo ambaye alikuwa na tatizo kwenye mkono na alipokelewa katika Kitengo cha Dharura na kuanza kupatiwa matibabu lakini tayari alikuwa amechelewa hivyo kuhitajika upasuaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live