Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyebakwa na kutobolewa macho aendelea kupokea faraja

30852 KIPOF+PIC TanzaniaWeb

Mon, 10 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kahama. Mwanamke Fatuma Maganga aliyebakwa kisha kutobolewa macho mwaka 2014, ameendelea kupatiwa misaada kutoka kwa wasamalia wema na taasisi mbalimbali.

Fatuma ambaye anaishi katika Kijiji cha Nyambula wilayani Kahama baada ya kufanyiwa kitendo hicho alitelekezwa na mumewe ambaye walikuwa wamezaa naye watoto 10.

Novemba mwaka huu gazeti la Mwananchi lilimtembelea mpaka nyumbani kwake na kuchapisha habari zake na tangu wakati huo amekuwa akitembelewa na watu tofauti.

Ofisa ustawi wa jamii wa mji wa Kahama Abdalahaman Nuru amesema Fatuma amepatiwa misaada mbalimbali ya chakula, malazi, kujengewa nyumba na watoto wake kugharimiwa huduma za shule.

Mkuu wa dawati la jinsia katika jeshi la polisi Kahama, Minael Kisagase amesema Jumatatu (kesho) siku ya kilele cha siku 16 za ukatili wa jinsia Fatuma atakuwapo na atatoa ushuhuda wa tukio hilo.

Pia alisema mbali na kutoa ushuhuda, mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamlingi Macha atamkabidhi kadi ya Benki ya NMB, akaunti aliyofunguliwa na wajasiriamali waliofika nyumbani kwake.



Chanzo: mwananchi.co.tz