Mwanamke mmoja mkazi wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Happyness William mwenye umri wa miaka 18 amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukiri kuiba kichanga cha miezi sita.
Mara baada ya kufikishwa katika mahakama ya wilaya ya Sengerema na kusomewa shtaka namba 64 la mwaka 2023 la wizi wa mtoto.
Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Sengerema Tumsifu Barnabas mshtakiwa huyo hakutaka kuisumbua mahakama akakiri kutenda kosa hilo ambalo alilitenda tarehe 26 ya mwezi huu alimuiba mtoto aitwaye Anitha Richard ili akamuonyeshe mume wake kuwa amejifungua na huyo ndiyo mtoto wake.