Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema dada wa aliyefariki baada ya kupata ajali na gari ya RC

70153 Dada+pic

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma.  Anastazia Shida,  dada yake Kasobi aliyefariki dunia jana usiku Jumatatu Agosti 5, 2019 baada ya kupata ajali akiwa anaendesha gari la mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema kaka yake alikuwa na leseni ya udereva aliyoipata Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta).

Akizungumza na Mwananchi kwa masikitiko leo Jumanne Agosti 6, 2019, Anastazia amesema hadi sasa hafahamu chanzo cha ajali iliyochukua uhai wa kaka yake.

“Ningependa kujua ajali hii imesababishwa na kitu gani. Nilitamani kujua kama ni mwendo kasi, hitilafu kwenye gari lakini nimeshindwa kwa kuwa tangu alipopata ajali juzi Jumapili hakuweza kueleza mazingira ya ajali,” amesema Anastazia.

Kasobi Shida alilazwa Hospitali ya Mkoa wa Mara Jumapili Agosti 4, 2019 baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari linalotumiwa na baba yake, Shida Masaba kumwendesha Malima.

Katika maelezo yake Anastazia amesema alionana na kaka yake muda mfupi kabla ya kufariki lakini alishindwa kumueleza chochote kutokana na kuwa na maumivu makali.

“Baada ya (Kasobi) kuhitimu mafunzo ya udereva Veta alikuwa tu nyumbani akisaidia kazi mbalimbali, pia alikuwa shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na hilo lilimfanya awe maarufu.”

Habari zinazohusiana na hii

“Pale hospitali tulielezwa kuwa alikuwa na tatizo tumboni, tulitakiwa kusubiri kuelezwa kama upasuaji ungefanyika pale au angepelekwa Hospitali ya Bugando lakini baadaye tulipewa taarifa kuwa amefariki dunia,” amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz