Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema RC Kungene baada ya maji kuongezeka Mto Ruvu

WhatsApp Image 2021 11 20 At 8.30.40 AM.jpeg RC Kunenge aipongeza Bodi Wami Ruvu, maji yakiongezeka Mto Ruvu

Sat, 20 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema amepokea taarifa kutoka Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwa wamewasha Mtambo wa Kuzalisha Maji wa Ruvu Chini baada ya Maji kuongozeka Mto Ruvu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipotembelea shamba la raia wa China aliyekamatwa na bonde hilo kwa kosa la kuvuta maji kutoka Mto Ruvu bila kibali.

Amesema kutokana na agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kufatilia sehemu ambazo zimechepushwa Maji na kuyaruhusu kuingia mtoni kumezaa matunda.

"Napenda kuwapongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kwa kufanya doria ambayo imezaa matunda kwani nimepokea taarifa kutoka DAWASA kuwa maji yameongezeka katika mtoni na kupelekea kuwasha mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini na pia bodi imethibitisha Maji kuongezeka kutoka mita 0.20 mpaka 0.61 kwa leo mchana.

Kufuatia hali hiyo ametoa agizo la kusitisha shughuli za kilimo kwa wakulima wa kilimo cha umwagiliaji waliokuwa wanatumia maji ya Mto Ruvu.

Kunenge amesema ni marufuku kwa mtu yeyote kuendelea kutumia maji ya Mto Ruvu kwa shughuli za umwagiliaji na mifugo hadi pale Serikali itakapotoa taarifa nyingine.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye aliongozana na kamati ya ulizi na usalama ya mkoa, Wilaya ya Bagamoyo na Kibaha pamoja na Maafisa kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wameshuhudia baadhi ya wakulima wakiendelea na shughuli za kilimo.

"Wakulima wote wenye vibali vya kutumia maji kwenye Mto Ruvu wasitishe shughuli zao hadi pale yatakapotoka maelekezo mengine, wanaonyweshq mifugo na kutumia mashine pia waache mara moja kwani kwa kuendelea kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya wananchi" amesema.

Imeandikwa na Frank Monyo na Julieth Mkireri

Chanzo: www.tanzaniaweb.live