Mwanza. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amemsihi Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo, Profesa Adelardus Kilangi kuwa mtulivu wakati wa kipindi kigumu cha kuondokewa na mkewe Natalia.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 7, 2019 wakati akiongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika ibada ya mazishi ya Natalia katika kata ya Luchelele wilayani Nyamagama jijini Mwanza.
Majaliwa amesema Serikali ipo na yeye (Kilanga) katika kipindi hiki kigumu.
"Mheshimiwa Rais (John Magufuli) amepokea msiba huu kwa huzuni kubwa, ameniagiza ni mwakilishe alitamani kuwapo lakini kulingana na majukumu aliyonayo ya ugeni wa SADC ameshindwa kufika," amesema
"Professa Kilangi anafanya kazi vizuri sana, kwa weledi na upole lakini alikuwa akipata utulivu kutokana na uwapo wa mama Natalia.”
Majaliwa amesema, "Jambo hili ni zito sana huwezi kulipokea kwa haraka hata nasi limetugusa sana, wajibu wetu sisi waombolezaji ni kumuombea marehemu lakini pia kumuombea Professa Kilangi apate utulivu.'
Pia Soma
- Ushirika Dar watoa ushauri serikalini, watofautiana hesabu za fedha
- LHRC yatafuta mbinu za kudumisha usawa kwa wenye ulemavu
- Mkapa kufunda vijana masuala ya uongozi na siasa za SADC