Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa amekufa ndani ya boma

Mauaji Mwanza Akutwa amekufa ndani ya boma

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja ambaye majina yake hayajafahamika pamoja na sehemu anayoishi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 -30 amekutwa ndani ya boma la nyumba akiwa amefariki huku mwili wake ukiwa umeharibika sana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Ally Kitumbo amesema baada ya kwenda kuuchukua mwili wa Kijana huyo ulionekana hauna majeraha yoyote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Geita ukisubiri uchunguzi wa Daktari.

Aidha Kitumbo amesema mpaka sasa chanzo cha kifo cha Kijanaa huyo hakijatambulika huku Jeshi la Polisi likiendelea kufanya uchunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live