Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa amefariki kwenye bwawa katikati ya msitu

Kifo Mauaji Wachimbaji Madini?fit=640%2C426&ssl=1 Akutwa amefariki kwenye bwawa katikati ya msitu

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 - 35 amekutwa amefariki katika bwawa dogo lililopo katika msitu wa Tanwat eneo la Kibena mjini Njombe.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni walinzi katika Msitu ya Tanwat uliyopo karibu na bwawa hilo wamesema kuwa mnamo majira ya saa 11:10 alfajiri ya leo, Novemba 21, 2022.

Waligundua uwepo wa mtu ambaye alikuwa kisogea katika bwawa hilo huku akiwa ameshika tochi na baada ya kufika akaanza kuingia ndani ya bwawa hilo na hata walipojaribu kumuita ili atoke nje ya bwawa hakuwasikiliza.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuutoa mwili katika bwawa, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Njombe Inspector Joel Mwakanyasa.

Huyu hapa ni miongoni mwa askari kutoka Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoani Njombe, anaeleza namna walivyofanikisha kuutoa mwili huo katika maji.

Baada ya mwili huo kutolewa katika bwawa Jeshi la Zimamoto liliwataka wananchi kuutambua mwili huo lakini wananchi akiwemo George Mlangwa wamekiri kutomfahamu mtu huyo.

Kufuatia tukio hili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Njombe limewaasa wananchi kuacha mara moja tabia ya kusogelea maji yenye kina kirefu ikiwa hawana uwezo wa kuogelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live