Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa usiku wa manane akichoma nyama ya Kondoo Makaburini

Nyama Ya Kondoo Akamatwa usiku wa manane akichoma nyama ya Kondoo Makaburini

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja ambaye majina yake hayajatambulika amekamatwa akiwa anachoma nyama aliyesema ni ya kondoo katika eneo la makaburi ya Pasua katika manispaa ya Moshi.

Mtu huyo ambaye licha ya kuchoma nyama amekutwa na vitambulisho vya watu wawili tofauti wakazi wa Dodoma na shanga ameshindwa kujieleza baada ya kukamatwa na walinzi wa makaburi.

Akizungumzia tukio hilo mlinzi wa makaburi hayo Juma Ngaini amesema mtu huyo aliwasha moto kwa muda mrefu kwa kutumia majani makavu huku akidai amekuja kupata dawa.

Jeshi la polisi limemchukua na vitu vyake kwa mahojiano zaidi.

Tazama Video hapa chini;

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live