Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na nyara za Serikali, yamo mafuta ya simba

Nyara Nyara Akamatwa na nyara za Serikali, yamo mafuta ya simba

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa Katavi linamshikilia mkazi wa Ilunde wilaya ya Mlele, Seda Mbutula (47) kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni mafuta ya Simba na ngozi yake akiwa amezificha kwenye mfuko nyumbani kwake.

Mbali na Nyara hizo za Serikali lakini mtuhumiwa huyo anadaiwa pia kukamatwa akiwa na ngozi ya Kakakuona, ngozi ya paka pori, vipande vinne vya meno ya ngiri na mkia wa nyumbu ambavyo kwa mujibu wa sheria ni nyara za Serikali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Ally Makame alitoa taarifa hiyo leo Novemba 27, 2021 wakati akizungumza na wanahabari kutoa taaarifa ya mafanikio ya operesheni waliyoifanya na kuwakamata watuhumiwa wa mkosa mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, alisema Mbutula alikamatwa Novemba 23,2021 saa 9:02 alasiri katika Pori la Akiba la Rungwa lililopo kata ya Ilunde na alikuwa ameficha nyara hizo ndani ya nyumba yake na kwamba anaendelea kuhojiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live