Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiua kisa kusumbuliwa na sauti za watu

Mauaji Nn.jpeg Ajiua kisa kusumbuliwa na sauti za watu

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja aitwae Emmanuel Kasapa (60) wa Mtaa wa Legezamwendo Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora amejiua kwa kujinyonga baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na sauti za Watu wasiojulikana zikimuamuru ajiue.

Watoto wa marehemu wamesema Baba yao amejaribu kujiua mara kadhaa akilalamika kusikia sauti za Watu asizozielewa zikimuamuru ajiue.

Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kariakoo Fredrick Itogoza amesema marehemu kabla ya kujiua sasa, alijaribu kujiondoa uhai kwa kunywa sumu miezi mitatu iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live