Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajinyonga kwa msongo wa mawazo

Vifo Idadi ya Vifo kwa kujinyonga imekuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari mara kwa mara

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja aliefahamika kwa jina la Majani James, ambae ni mlemavu wa miguu amekutwa amefariki, huku akining'inia kwenye kamba nyuma ya nyumba yake.

Inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliyekuwa akiishi katika Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neruma, Wilaya ya Bunda mkoani Mara, alijinyonga kutokana na msongo wa mawazo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tubishubwamu, amesema kuwa mlemavu huyo mjasiriamali amejinyonga majira ya saa 12 asubuhi kijijini hapo.

Kamanda Tubishubwamu amesema Mwananchi huyo aliyekuwa na kibanda cha biashara, pia alikuwa fundi cherehani kijijini hapo.

Taarifa zinasema siku moja kabla ya tukio hilo kulikuwa na kikao cha wanafamilia na wana ukoo kujadili mwenendo wa James kimaisha.

Taarifa ya Polisi imesema wakati wakipekua kwenye mfuko wa nguo ya marehemu walikuta karatasi iliyokuwa na maandishi kwamba asisumbuliwe mtu yeyote kuhusu kifo chake, kwani ameamua kujitoa uhai wake yeye mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo.

Aidha Kamanda Tubishubwamu ametoa wito kwa wananchi wamrudie Mungu na wanapopata changamoto zikiwemo za kimaisha waombe ushauri kwa wenzao na viongozi wa dini.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali teule ya Halmashauri ya mji wa Bunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live