Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajinyonga kisa kukosa pesa ya kwenda msibani

Mauaji Kiteto Mkd Ajinyonga kisa kukosa pesa ya kwenda msibani

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wilison Bahati mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kijiji cha Kashelo wilaya ya Mbongwe mkoani Geita amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa madai ya kukosa nauli ya kumpa mke wake ili wasafiri kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ukweni kwake.

Akizungumza nasi, Grace Jeremia ambaye ni mke wa marehemu amesema kuwa, "Mume wangu alijinyonga kwa sababu alikosa hela ya kwenda msibani nyumbani kwetu ilikuwa saa 11:00 asubuhi aliniacha nimelala akavaa nguo akasema naenda shambani ndiyo tukamkuta sasa ameshajinyonga.

"Tulikaa pamoja nyumbani tukazungumza lakini alisema hela amekosa sasa sijui alipata huzuni ndo akachukua uamuzi wa kujinyonga."

Kwa upande wake Baba wa marehemu amesema kuwa, "Nilikuwa sipo nyumbani nikapata taarifa mtoto wako amefariki nikauliza amefariki kivipi wakaniambia amefariki kwa kujinyonga.

"Yaani nilisikitika sana nikatoka huko nyumbani nilipokuwa ninaishi nikaja nikafika hadi kwenye tukio nikaanza kujiuliza hivi kwanini mtoto wangu ajinyonge sijui ni kwa ajili ya majungu ya watoto wangu yaani nasikitika kwakweli."

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amesema alitoa taarifa kituo cha polisi na askari walifika na kufanya uchunguzi wa tukio hilo na baadae familia ikaruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: