Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajaribu kujiua kwa moto wa petrol

Moto Petrol Sddca Ajaribu kujiua kwa moto wa petrol

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wa familia Moja wamenusurika kifo baada ya Nyumba waliokua wakiishi kutekekea kwa Moto unaodaiwa kusababishwa na Mmoja wa wanafamilia hao kujimwagia mafuta ya Petroli kwa Dhumuni la kujiua.

Miongoni mwa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Augustino Elius ameeleza ndugu yao Pascal Elius (mtuhumiwa) aliwaita ndani wakiwa watatu na mtuhumiwa wa nne Ili awaeleze changamoto zake za kiafya lakini ghafla alichukua mafuta ya Petroli na kujimwagia na kuepekea nyumba kuteketea kwa moto na kusababisha wote wanne kujeruhiwa kwa kuungua sehemu mbalimbali za Miili yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Alex Mkama, ameeleza tukio hilo la Moto limetokea kijiji cha Gonja kata ya Pemba wilaya ya Mvomero, ambapo kwa sasa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo wakati majeruhi hao wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro huku mtuhumiwa akiendelea kupatiwa matibabu chini ya ulinzi.

Kwa upande wake Muuguzi wa Zamu Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro Devotha Msungus amesema majeruhi hao wamepata majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao, wawili kati yao wamelazimika kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi na Wawili wanaendelea kutibiwa katika hospital hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live