Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua wawili Mbeya

Ajali Mbeya Tgh Ajali yaua wawili Mbeya

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Kyela Express kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster lililokuwa likisafirisha msiba kutoka mkoani Dodoma kwenda wilayani Kyela.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk. Vicent Anney, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo Jumanne Oktoba 11, 2022 majira ya saa 2.30 asubuhi katika kijiji cha Ibula Kata ya Kiwira.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo na mpaka natoka eneo la tukio kuna vifo vya watu wawili lakini kwa upande wa majeruhi bado sina idadi kamili nafuatilia ntakupa taarifa kamili,” amesema Mkuu wa Wilaya huyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kiwira wilayani Rungwe, Michael Simon, amesema basi la Kyela Express lilipopofika eneo la Kanyegere iligongana na gari aina ya Costa na watu waliopoteza maisha na majeruhi walikuwa ndani ya Costa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live