Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua watu watano Lindi

24102 Kamanda+pic TanzaniaWeb

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu watano wamefariki dunia na mmoja amejeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace kugongana na lori katika kijiji cha Likahakwa katika Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi leo Oktoba 25, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Prudenciana Protas amesema ajali hiyo imetokea asubuhi leo ikihusisha hiace iliyokuwa ikienda Lindi mjini na lori lililokuwa linaelekea Dar es salaam.

“Ni kweli ajali imetokea asubuhi na imesababisha vifo vya watu watano ambao walikuwa abiria kwenye hiace na majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa hiace hiyo,” amesema

“Baada ya ajali hiyo dereva wa lori ambalo ni mali ya Kampuni ya Dangote alikimbia na polisi bado wanamtafuta,” ameongeza

Kamanda Protas amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kupita upande wa haice  na kukukutana uso kwa uso.

“Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori ambaye alipita upande wa hiace ndipo wakakutana na ndiyo maana baada ya ajali dereva wa lori alikimbia,” amesema.

Amesema miili ya marehemu zimepelekwa katika Hospitali ya Sokoina pamoja na dereva wa hiace ambaye alijeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz