Watu watatu wamefariki na wengine wanne wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso Kijiji cha Mbala Vigwaza mkoani Pwani saa 3 usiku wa Oktoba 23, 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Octoba 24, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Pius Lutumo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari dogo aina ya Toyota Kluger lililokuwa likitokea Mkoani Iringa kuelekea Jijini Daresalaam
"Waliokuwa kwenye gari dogo walikuwa wanatoka Iringa kuelekea Dar es Salaam na huyu wa lori aina ya Scania alikuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro, lakini dereva wa gari dogo alikuwa na mwendo mkali bila kuchukua tahadhari," amesema.
Amewataja waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa pamoja na moja Mbuma anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (35-40), Pokera (19) wote wakazi wa Mbezi Dar es Salaam na Mwanahamisi (18) mkazi wa Kijitonyama jijini humo.
Amewataja pia majeruhi kuwa ni pamoja na Amina Kondo mkazi wa Manzese Daresalaam, Abdallah Ally na majeruhi wawili ambao bado hawajtambulika majina yao.
Lutumo amesema kuwa miili ya marehem hao imehifadhiwa kwenye Hospital ya Lugoba na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospital ya Msoga Mkoani humo mkoani Pwani.