Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua watano Kigoma, wamo mafundi umeme

Ajali Watano Kigoma Ajali yaua watano Kigoma, wamo mafundi umeme

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Watu watano wamefariki dunia na wengine wanane wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Philemon Mkungu amesema leo Jumatatu Juni 10, 2024 kuwa ajali hiyo ilitokea jana eneo la Katare, kijiji cha Rukoma wilayani Uvinza, ikihusisha gari aina ya Fuso mali ya kampuni ya Tropical/State Grid co. LTD inayosambaza umeme vijijini.

Kamanda Makungu amewataja waliofariki dunia ni kuwa ni Samweli Zakaria (30), Dismas Meshack (21), Juma Bashiru(29) ambao ni wakulima na wakazi wa Wilaya ya Uvinza na mafundi umeme, Enock Chimangulu (42), mkazi wa mkoani Tanga na Benson Thomas(25), mkazi wa Arusha.

Kamanda Makungu amesema gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Said Ramadhani ikitokea kijiji cha Lubisi kuelekea kijiji cha Rukoma, iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo hivyo na majruhi ambapo kati yao majeruhi watatu wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Amesema majeruhi wengine watano wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni wakiendelea kupatiwa matibabu ambao ni Hussein Fadhili (24) msimamizi wa mradi na mkazi wa mkoani Tanga, Yasini Athumani(19) kibarua na mkazi wa Uvinza.

Wengine ni Mtala Joseph(24), mkazi wa Musoma, mkoani Mara, Victor Josph(31) pamoja na Claudiao Mwalima(31) mkazi wa Mkoa wa Mbeya ambao ni mafundi umeme.

“Majeruhi watatu waliopatiwa matibabu na kuruhusiwa ni pamoja na Said Ramadhani(45), ambaye alikuwa dereva wa gari hilo, Elizabeth Mero (30), msimamizi wa mradi wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam pamoja na Venance Mabura (24), fundi umeme na mkazi wa mkoani Geita,”amesema Kamanda Makungu

Chanzo: Mwananchi