Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua watano Bagamoyo

Ajali Mdkld Ajali yaua watano Bagamoyo

Sun, 8 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watano wamefariki Dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye eneo la Mwavi Kiwanga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema miili ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Bagamoyo huku majeruhi kumi wakidaiwa kuwa katika hali mbaya hospitalini hapo.

Ajali hiyo iliyotokea wilayani Bagamoyo imetokea leo asubuhi ikihusisha gari aina ya Coaster inayofanya safari zake kutoka Bagamoyo kwenda Morogoro yenye namba za usajili T 972 BTY Toyota iliyogongana uso kwa uso na Kenta Mitsubishi yenye namba za usajili T168 EAZ.

Licha ya kutokea kwa vifo na majeruhi, abiria wengine kadhaa walipata michubuko katika ajali hiyo na wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao baada ya kupatiwa matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live