Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua walimu watatu Mbeya

28809 AJALI+PIC TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Walimu watatu kati ya saba wa Shule ya Sekondari Lupoto ya wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya wamefariki na wengine wanne wamepata majeraha baada ya gari aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria kupata ajali barabara ya Matema kwenda Kyela mjini mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amewataja walimu waliofariki ni David Edwin, Mashaka Mkalafu ambao walifia eneo la tukio na Robert Mwakasaka  alifia Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Happy Sichone, Lameck Sanga, Stiven Kahaya na Lazack Lwesya ambao walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Amesema walimu hao walipata ajali hiyo jana saa 12:50 jioni katika Kijiji cha Bwato barabara ya Bwato kwenda Matema wilayani Kyela wakati wakitoka Matema Beach, Ziwa Nyasa walikokwenda kwa ajili ya matembezi.

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva  lakini pia dereva huyu alikuwa mgeni na barabara ile  ambayo bado ipo kwenye matengenezo na dereva aliyetambuliwa kwa jina la  Ambonisye Mwankeja alikamatwa na yupo mahabusu-Kyela,” amesema Kamanda Matei.



Chanzo: mwananchi.co.tz