Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua saba, watano wafanyakazi Azam TV

65954 Pic+azam+tv

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8, 2019 eneo la Shelui mkoani Singida wakati wakieleleka wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.

Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.

“Katika basi hilo dogo wafanyakazi walikuwa kumi, watano wamejeruhiwa,” zinaeleza taarifa hizo.

Uzinduzi wa Hifadhi hiyo unafanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz