Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua Morogoro

Ajali Morogoro.png Ajali yaua Morogoro

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Millard Ayo

Mtu mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari la abiria aina ya Tata lenye namba za usajili T 596 EAF linalofanya safari zake Morogoro - Mlimba kugongana uso Kwa uso na bajaji iliyokuwa inatokea Mindu kuelekea Morogoro Mjini.

Mmoja wa Majeruhi hao Angel Zacharia amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Mindu Barabara kuu ya Morogoro - Iringa mapema leo huku chanzo chake kikiwa ni uzembe wa Dereva wa basi la abiria kuhama upande wake bila kuchukua tahadhari na kuigonga bajaji hiyo.

Daktari Kutoka kitengo cha dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Joseph Kwai amekiri kupokea mwili wa marehemu ambaye ni Mwanamke aliyekuwa abiria wa bajaji huku majeruhi hao wakitokea kwenye basi na bajaji. #MillardAyoUPDATES

Chanzo: Millard Ayo