Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya ndege Bukoba: Miili ya watumishi wa MDH yaagwa Dar

FFFA Miili ya watumishi wa MDH waliofariki kwenye ajali ya ndege Bukoba

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya waombolezaji hasa wafanyanyazi wa MDH  wamejitokeza katika (hafla) zoezi la utoaji wa heshima za mwisho kwa watumishi wa MDH walifariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea Novemba 6, 2022 Bukoba Mkoani Kagera. 

Rashid Mfaume Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akimwakilisha Waziri wa Afya anabainisha kuwa watumishi hawa wamekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa MDH akaeleza namna watumishi hao walivyoacha pengo kubwa, kutoka na mchango wao mkubwa katika kuhakikisha watu wanakuwa na afya nzuri. 

Watumishi walioagwa jana jijini Dar es salaam, walifariki asubuhi ya Novemba 6,2022 katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la precision Bukoba Mkoani Kagera. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live