Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya magari matatu yaua mmoja Morogoro

Ajali Moro 2e.jpeg Ajali ya magari matatu yaua mmoja Morogoro

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 33 kunusurika mara baada ya ajali iliyosisha magari matatu ikiwemo gari ndogo ya NISSAN MISTUBISH yenye usajili namba T846 CWN, lori na Basi kampuni ya BM COACH yenye namba ya usajili T 959 DDE kugongana katika eneo la Makunganya Barabara Kuu ya Morogoro - Dodoma.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Ahamedi Lemba amesema ajali hiyo imetokea majira ya mchana na kusababisha kifo cha dereva wa gari dogo Alphonce aliyekuwa akitokea Morogoro kwenda Dodoma kubanwa na magari mawili na kusababisha kifo hicho.

Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa roli kusimamisha lori lake katikati ya barabara na kusita kuendelea mara baada ya kutaka kuyapita magari mwngine na kusabisha gari dogo la MISTUBISH kubanwa na basi la kampuni ya BM COACH.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live