Tukio limetokea #Mikumi eneo la Ruaha Mbuyuni ikihusisha Gari ndogo pamoja na Lori ambapo Watu wengine watatu wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Mikumi kwa matibabu ambapo mmoja ameruhusiwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ALex Mukama aliyethibitisha kutokea kwa vifo vinne na majeruhi watatu ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Mikumi kwa Matibabu ambapo mmoja wao karuhusiwa.
"Ni kweli ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajiri baada ya gari ya Magazeti aina ya Noah iliyoparamia Lori lililokuwa limeharibika na kulingonga kwa nyuma."
Kamanda Mukama amewashauri Madereva kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani na kuendesha vyombo vyao kwa mwendo unaruhusiwa ili kuepusha ajali zisizo za lazima.