Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya Pwani: Watatu wajitokeza kupimwa DNA, Muhimbili yawaita wengine

73924 DNA+PIC

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ndugu wa marehemu watatu kati ya watano wa ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia juzi Jumamosi Agosti 31, 2019 Kibiti mkoani Pwani wamejitokeza kuchukuliwa sampuli kwa ajili ya kipimo cha utambuzi wa vinasaba (DNA).

Jana Jumapili Septemba 01, 2019 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam ilitoa wito kwa ndugu kujitokeza kupima DNA ili kuwatambua miili ya wapendwa wao ambao imeharibika.

Miili ya watu hao watano, minne ni ya watu wazima na mmoja mtoto ilifikishwa katika hospitali hiyo juzi Jumamosi asubuhi kwa ajili ya kuhifadhiwa ikiwa haitambuliki kutokana na kuharibika.

Ofisa uhusiano wa MNH, Sofia Mtakasimba akizungumza na Mwananchi amesema hadi kufikia leo Jumatatu Septemba 2, 2019 saa nane mchana ndugu wa watatu ndiyo waliofika kuchukuliwa sampuli ili kupima DNA.

“Sampuli zimeshachukuliwa kwa ndugu wa maiti tatu, wamebaki wawili tunaomba nao wajitokeze ili zoezi la kuwatambua lifanyike,” amesema

Uamuzi wa  kufanya kipimo hicho ulifikiwa baada ya miili hiyo kuharibika na kushindwa kutambulika kutokana na kuungua moto.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement   ?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga akizungumzia ajali hiyo juzi Jumamosi alisema ilihusisha lori la kampuni ya Dangote lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mtwara likiwa limepakia malighafi ya kutengeneza saruji.

Lori hilo liligongana na gari dogo aina ya Toyota Premio lililokuwa likitoka kwenye nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Kibiti eneo la Kinyanya.

Alisema gari hilo liliingia barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Mtwara bila kuzingatia sheria na kugongana na lori hilo.

Kamanda Lyanga alisema  baada ya magari hayo kugongana gari la Dangote lilipoteza mwelekeo na kugonga nguzo ya umeme na nyaya kuanguka iliyosababisha moto ulioshika katika lori hilo na kusababisha vifo vya watu wanne na mmoja kati ya watu wawili waliokuwa katika gari hilo dogo alifariki  wakati akipatiwa matibabu wilayani Rufiji mkoani Pwani.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz