Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya Fuso yaua watu 13 Songea

Ajali Kapricon Fds Ajali ya Fuso yaua watu 13 Songea

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

Watu 13 wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Fuso waliyokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni majira ya saa 2: 30 usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema gari hiyo ilikuwa imebeba wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani katika kijiji cha Ndongosi na walikuwa wakielekea kijiji jirani cha Namatuhi wilayani humo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Songea na tayari ndugu wameitambua miili hiyo. DC Ndile amesema majeruhi wanaendelea na matibabu katika kituo cha Afya cha Namanditi.

Chanzo: Habarileo