Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya Bus dereva akimbia, mtoto afariki, 23 wajeruhiwa

4574cdfec3a98e139d7d29f04c378158 Ajali ya Bus dereva akimbia, mtoto afariki, 23 wajeruhiwa

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MTOTO mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi mwenye umri unaokadiriwa kuwa ni miaka 7,amefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Frester, linalofanya safari kati ya Kahama na Musoma, ambapo mara baada ya ajali kutokea dereva wa basi hilo alikimbia.

Ajali hiyo imetokea leo Desemba 17, 2020, majira ya saa 12:00 asubuhi, katika eneo la Nyakato nje kidogo ya mji wa Kahama, likiwa kwenye mwendokasi muda mfupi tu baada ya Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa, kulikagua basi hilo na kuliruhusu kuendelea na safari.

Akizungumza Kamanda Mutafungwa, anasema alikutana na madereva wa mabasi yote yaendayo mikoani kabla ya kuanza safari na kuwakumbusha kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha kwa mwendokasi.

"Haiwezekani upatiwe elimu ya usalama barabarani halafu muda huo huo ukiuke sheria na kusababisha ajali huu ni uzembe, kwani amesababisha kifo na kujeruhi watu 23 tutachukua hatua kali dhidi yake pindi atakapokamatwa", amesema Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa, amesema basi hilo lilikuwa na abiria 47 ambapo 23 wamejeruhiwa na watatu hali zao sio nzuri huku wengine wakiruhusiwa kuendelea na safari baaada ya kupata michubuko ambapo kampuni hiyo ililazimika kuwatafutia usafiri mwingine na kuendelea na safari kwenda mkoani Mara.

Chanzo: habarileo.co.tz