Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali basi la Kemebos yaua mwanafunzi, yajeruhi sita

Kemmos Bus Ajali basi la Kemebos yaua mwanafunzi, yajeruhi sita

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Mwananchi

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kemobos, Frank Makage (17) amefariki dunia na watu wengine sita, wakiwemo wafanyakazi wa shule hiyo wakijeruhiwa kwenye ajali ya basi iliyotokea Kata ya Kimwani wilayani wilayani Muleba mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea leo Machi 24, 2024, wakati wanafunzi 35 wa shule hiyo walipokuwa wakisafirishwa kwenda kwenda likizo fupi ya muhula wa kwanza Katoro mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya Muleba, Dk Abel Nyamahanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema imetokea usiku wa manane.

"(Basi) Lilikuwa limebeba wanafunzi, limepata ajali usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane usiku na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wenzake sita kupata majeraha," amesema Nyamahanga.

Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba mkoani Kagera, Asheri Mpango amethibitisha kupokea mwili wa mwanafunzi huyo na majeruhi sita, wakiwamo wanafunzi pamoja na watumishi wa shule hiyo.

"Umepokelewa mwili wa mwanafunzi mmoja, majeruhi sita na mmoja wao, Anitha Frederick ambaye ni matroni amevunjika mkono. Pia yumo mfanyakazi mwingine aitwaye Ashraf Athman (21) na Magdalena Muhage (16) ambaye ni mwanafunzi," amesema Mpango

Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Bracius Chatanda amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mei 6, 2017 ajali mbaya ya gari ilitokea kaskazini mwa Tanzania, ambapo basi aina ya Costa mali ya Shule ya Msingi Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo, lilitumbukia katika Mto Marera katika Mlima Rhotia, Karatu mkoani Arusha.

Mkasa huo ulisababisha vifo vya wanafunzi 32 waliokuwa wanakwenda kufanya mtihani wa majaribio kwenye shule rafiki. Wanafunzi watatu walinusurika.

Chanzo: Mwananchi