Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali Boma: Gari latumbukia mtoni na kujeruhi 19

Ajali Mbaya Ault (1) Ajali Boma: Gari latumbukia mtoni na kujeruhi 19

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 19 wameheruhiwa na wengine watano hali zao ni mbaya baada ya gari ya abiria aina ya Coaster waliyokuwa wanaitumia kusafiri kutokea Arusha kwenda Moshi kuangukia nakupindukia katika mto wa kijiwe cha mtoni baada ya Fuso kuigonga gari hiyo katika mji wa Bomang’ombe,Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Abiria aliyenusurika kwenye ajali hiyo amesema alikuwa akienda kazini Moshi lakini alisikia kishindo kizito…“Nilisikia kama dereva alikuwa anakwepa baada ya kile kishindo niliduaa nikatoka mwenyewe,vioo vimeingia kwenye mkono nimeshonwa na mguu umeumia,” amesema Husein Selemani.

Kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Saimon Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari aina ya Fuso kutaka ku overtake sehemu isiyofaa nakuigonga coaste nakupinduka nakusababisha majeruhi ya watu 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live