Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali Biharamulo yaua watano

Index 2 Ed Ajali Biharamulo yaua watano

Sun, 1 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ajali hiyo imeyahusisha gari la abiria lenye namba za usajili T567 DFA mali ya kampuni ya Frester lililokuwa likitoka mkoani Morogoro kuelekea Bukoba mkoani Kagera, baada ya kugongana na gari dogo aina ya Corora lenye namba za usajili T741 AXY lililokuwa likitoka wilaya ya Muleba kuelekea mkoani Geita.

Mganga Mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Dk. Gresmus Sebuyoya amesema wamepokea miili ya watu watano, ambayo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Dk. Sebuyoya ametaja majina ya marehemu hao kuwa ni Majid Abubakar, Mdathiru Hashim, Julian Julius, John Method na mwingine amefahamika kwa jina moja la Fravius, wote wanaume.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alikuwa akiendesha kwa kasi na kusababisha kuhama katika sehemu yake na kwenda kugongana uso kwa uso na gari hilo dogo.

Chanzo: ippmedia.com