Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali Babati: Gari latumbukia kwenye korongo na kuua

Ajali Msms Ajali Babati: Gari latumbukia kwenye korongo na kuua

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja (Dereva) amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika Kata ya Sigino Wilayani Babati Mkoani Manyara baada ya gari la abiria (Coaster) kufeli breki na kutumbukia korongoni.

Akiongea kwa njia ya simu RPC wa Manyara, George Katabazi amesema gari hilo lilikuwa linatokea Mkoani Singida kuelekea Arusha na baada ya kufika eneo la kona ya Logia ndipo likafeli breki na kumshinda Dereva.

“Ajali imetokea leo, gari lilikuwa na Watu 29 abiria ni 27 Dereva mmoja pamoja na utingo wake, Dereva amefariki huku majeruhi wakiwa saba ambapo kati yao watatu hali zao ni mbaya ila abiria wengine walipata mshtuko tu, chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa breki wa gari hali iliyopelekea kumshinda Dereva kulimudu gari hilo na kuingia kwenye korongo,” amesema RPC Katabazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live