Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajabu! Waachisha watoto shule wamsubiri Yesu

Wanafunzi Mtihani Necta.jpeg Ajabu! Waachisha watoto shule wamsubiri Yesu

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Millard Ayo

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amefanya msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule za Msingi na Sekondari Vijijini ambapo katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya ( 33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua Kanisa Kijijini hapo akiwahubira Wazazi wasiwapeleke Watoto Shule kwakuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda Shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni Kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri akaacha Chuo na kwenda kuanzisha Kanisa hilo Namtumbo “Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa Mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu, mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya Wazazi baada ya kujitambua Mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chap- ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu”

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni Wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato Kijijini hapo na wameachisha Watoto wao Shule ili wajiandae kumpokea Yesu ambapo hadi sasa Watoto 13 tayari wameacha kwenda Shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na Elimu Dunia inayotolewa na Shule za Serikali na binafsi.

Watoto wa Wasabato walioacha Shule na kujiunga na Kanisa hilo pamoja na Wazazi wao ili kumsubiri Yesu ni pamoja na Abigaili Anthony Mkomela (13), Rachel Antony Mkomela (9), Setianthony Slavio (2), Nathaniel Slavio (9), Irene Antony (18), Huria Antony Mkomela (6), Thabiti Mkomela ( 6), Seth Mkomela 6), Methew Makiluli ( 6), Lomanous Ngonyani (8), Sila Ngonyani (3), Bions Alfred (5), Lackson Alfred (8).

DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: Millard Ayo