Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Airport ya Mwanza yaandaliwa kuipokea ndege mpya Dreamliner 787-8

11381 Boei+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwele ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), kuufanyia ukarabati wa haraka uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa ajili ya uzinduzi wa safari za ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner Julai 29.

Mhandisi Kamwele ametoa maagizo hayo leo Julai 13 jijini Mwanza alipotembelea taasisi na kukagua miradi iliyoko chini ya Wizara hiyo.

Amesema Serikali pia itatekeleza ujenzi na ukarabati wa viwanja vingine tisa nchini kufikia viwango vya kuruhusu safari za ndege zote kubwa na ndogo.

Ametaja baadhi ya viwanja hivyo kuwa ni pamoja ni Songwe-Mbeya, Mtwara, Musoma, Kigoma, Songea, Shinyanga, Geita na Tabora.

Waziri huyo pia ameuagiza uongozi wa Shirika la ndege nchini (ATCL), kurekebisha mfumo wa ukataji wa tiketi, hasa kupitia kwa Mawakala ili kudhibiti ongezeko la bei kulinganisha ille inayotangazwa na shirikali hilo.

“Baadhi ya mawakala huwatoza wananchi kati ya Sh400, 000 hadi Sh500, 000 kwa safari kulinganisha bei inayotangazwa na shirika la Sh260, 000; nitoa muda wa wiki tatu mchezo huu ukomeshwe,” amesema.

Waziri huyo pia ametembelea bandari ya Mwanza pamoja na shirika la reli.

Chanzo: mwananchi.co.tz