Ndege kubwa ya Airbus A380 ya Shirika la Ndege la Emirates yenye uwezo wa kubeba Abiria 550 imetua kwa dharura Jijini Dar es salaam usiku huu katika uwanja wa Julius Kambarage Nyerere ikiwa na Abiria 514.
Chanzo cha kuaminika kimesema kuwa ndege hiyo ambayo imetokea Sao Paulo, Brazil kuelekea Dubai imetua kwa dharura ili kuongeza mafuta yatakayoisaidia kukamilisha safari yake ambayo sasa imerefushwa kutokana na kulazimika kuikwepa njia yake ya kawaida ambayo ilikua ni kupita kwenye anga ya Sudan ambayo kwa sasa imefungwa.
Hii sio mara ya kwanza kwa Ndege hii kubwa ya Abiria duniani kutua kwa dharura nchini Tanzania kwani mwaka 2018 Airbus A380 kama hii ilishindwa kutua nchini Mauritius kutokana na hali mbaya ya hewa na badala yake ikatua Dar es salaam Abiria wakalazwa Hotelini na kuondoka kesho yake.