Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aibiwa mtoto mchanga akiwa bafuni

Kichanga Pic Aibiwa mtoto mchanga akiwa bafuni

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Swaumu Mahondola mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kijiji cha Kibumba, wilayani Chato, mkoani Geita anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa mwezi mmoja na siku tatu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, imebainisha kuwa mnamo Disemba 22, 2023, majira ya saa tano usiku, Swaumu alimvizia mama wa mtoto huyo aitwaye Martha Phelemon, mkazi wa Kata ya Ludete iliyopo Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, alipoenda bafuni kuoga, ndipo alipomuiba mtoto huyo.

Hata hivyo Jeshi hilo limesema baada ya kumpata mtoto huyo alifanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika Kituo cha Afya cha Katoro na kuonekana ana afya njema na kwamba tayari amekabidhiwa kwa wazazi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live