Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally akutwa ameuawa nyumbani kwake

Shinyanga Re Ahmed Ally akutwa ameuawa nyumbani kwake

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyakazi wa bomba la mafuta na Mkazi wa Mtaa wa Nyasubi, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Ahmed Ally (56), amekutwa ameuawa na watu wasiojulikana nyumbani kwake kisha kuacha wamemfungia kwa nje.

Akisimulia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyasubi, Leonard Mayala, alisema taarifa za kutokea kwa kifo hicho alizipata kwa majirani ambao Ally alikuwa amepanga nao sehemu moja baada ya kusikia harufu mbaya.

Mayala alisema alifika kwenye eneo la tukio na kukuta mlango umefungwa kwa nje na harufu ikitokea dirishani, ndipo walipotoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kahama, ambao walikwenda kuvunja mlango na kukuta mwili wa mfanyakazi huyo umeanza kuharibika.

Baadhi ya mashuhuda na majirani wa marehemu, akiwamo Dumisha Kabaula, alisema mtu huyo alitokea Dar es Salaam kuja Kahama kufanya kazi, lakini siku kadhaa bila kwenda kazini na alipomwuliza alidai anaumwa, na siku hiyo alikuwa ajiandaa kuhama lakini baada ya siku nne wakapata taarifa za kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live