Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la Waziri Ndumbaro la wakaba Kilimanjaro

KANAPAww Agizo la Waziri Ndumbaru la wakaba Kilimanjaro

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: mwananchidigital

Sheria inayozuia wananchi wanaoishi vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro (Kinapa) kuingia kwenye msitu wa nusu maili kuokota kuni na majani, imegeuka kaa la moto kwa wananchi hao.

Hii ni baada ya uongozi wa Kinapa kuanza kutekeleza sheria hiyo na baadhi ya wananchi kukamatwa wakiwa ndani ya hifadhi, licha ya kupewa elimu ya katazo la kuingia hifadhini.

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambayo ni moja ya urithi wa Dunia inapakana na vijiji 92 vilivyopo wilaya za Rombo, Hai, Siha na Moshi mkoani Kilimanjaro na wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha.

Huko nyuma, msitu huo ulisimamiwa na Idara ya Misitu, lakini Septemba 16, 2005 uliingizwa chini ya usimamizi wa Kinapa chini ya sheria namba GN 278 baada ya kubainika kukithiri vitendo vya uharibifu wa mazingira.

Mwaka 2014 kikao cha mashauriano mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kiliazimia wanawake wawe wanaingia katika msitu huo kuokota kuni na kukata majani kwa ajili ya malisho na muda huo ulimalizika mwaka 2019.

Licha ya kumalizika kwa muda huo, wananchi bado wanaona ni haki yao kuingia katika eneo hilo kwa ajili ya shughuli za kibinadamu kama kukata kuni na majani, jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa Kinapa. Dhamira ya Serikali kupitia kikao cha RCC ilikuwa wananchi waruhusiwe kuingia kuokota kuni na kukata majani, lakini na wao wawe walinzi, lakini imekuwa tofauti na uharibifu ni mkubwa.

Baada ya kumalizika kwa ahueni hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaru alifanya ziara mkoani Kilimanjaro Julai 14 mwaka huu na akatangaza hakuna mwananchi ataruhusiwa tena kuingia hifadhini.

Kuanzia wiki iliyopita, wanasiasa na wananchi wameanza kupaza sauti kupinga kukamatwa kwa watu wanaoingia hifadhini wakitoa tuhuma za askari wa Kinapa kukiuka haki za binadamu wakati wa ukamataji.

Mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei amewataka wananchi kutekeleza agizo la Waziri Ndumbaro wakati wakitafuta njia za kuhakikisha agizo hilo linarekebishwa na Serikali.

Chanzo: mwananchidigital