Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la RC Makalla kwa hospitali zinazouia maiti kisa madeni

Makalla3 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesisitiza agizo lililotolewa na Wizara ya Afya linalokataza Hospitali kuzuia maiti kuchukuliwa na ndugu kwa kigezo cha deni.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema hayo baada ya kupokea malalamiko toka kwa Wananchi kuwa bado kuna hospitali hazitekelezi agizo hilo la Wizara na Kuendelea kuzuia maiti mpaka zilipiwe fedha za matibabu zilizokwisha tumika.

Hata hivyo kitendo hicho kinapelekea vyumba vya kuhifadhia maiti kukosa nafasi kutokana na hospital nyingi kukatalia maiti.

Aidha, Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live